WhatsApp kuna kipengele cha kufuta ujumbe ambao tayari umeutuma kwa mtu sio?–Delete For Everyone– na kipengele hiki ili kifanikiwe kwa pande zote mbili inabidi uwahi kufanya hivyo kabla muda Fulani kupita..
WhatsApp Imekua na maboresho na uongezaji wa vipengele kadha wa kadha, soma Zaidi >>HAPA<<
Muda ukiongezwa katika kipengele hichi basi hii itakua imesaidia sana watu na pengine hata kuwaepusha na kuchukuliwa vibaya na upande wa pili.
Pata picha kipengele kama hichi kikiwa kimeongezwa muda labda kwa masaa 12 au hata siku mbili? Hii itakua na tija Zaidi sio?
Hapo awaili ulikua na uwezo wa kufuta meseji ndani ya dakika nane tuu baada ya kutuma ujumbe huo, muda huo ukipitiliza basi ujumbe utashindwa futika upande wa pili.
Huduma zingine za kutuma na kupokea meseji katika mitandao ya kijamii kama vile instagram zenyewe hazina muda maalumu wa kufuta –unaweza kufuta muda wowote–jumbe hizo.
WhatsApp kwa sasa inakuja na vipengele vingi vipya vipya au kuboresha baadhi ya vipengele ambavyo mwanzoni havikuwepo kabisa katika mtandao huo.
Kipengele hiki kwa sasa kipo katika hatua za mwanzo mwanzo na kinafanyiwa majaribio kwa baadhi ya wadau waliochaguliwa, muda si mwingi kitatoka na kuanza kutumika kwa watu wote
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je hili umelipokeaje? Je kipengle hichi kitakusaidia kwa namna moja au nyingine?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.